• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

Imetumwa : May 18th, 2025

Na Sofia Remmi.

Habari:Dodoma Rs.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule, amefungua Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Nyuki Duniani leo tarehe 18 Mei 2025 katika Bustani ya Mapumziko ya Chinangali ( Chinangali Park) Jijini Dodoma.

Akizungumza na wananachi pamoja na wadau wa Nyuki Mhe. Senyamule amesema Dunia nzima huadhimisha Siku ya Nyuki ambayo ni matokeo ya makubaliano ya Baraza la Umoja wa Mataifa mnamo Mwaka 2017.

Lengo kuu la kuanzishwa kwa madhimisho haya ni kutambua mchango wa Sekta ya Nyuki katika maisha ya mwananchi mmoja mmoja, Taifa na Dunia kwa ujumla,Siku hii ni sehemu ya kuenzi jitihada za mwanzilishi wa ufugaji Nyuki Bwana Anton Janša raia wa nchi ya Slovenia ambapo Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ziliidhinisha na kutangaza rasmi tarehe 20 Mei ya kila mwaka kuwa siku ya Nyuki Duniani itakayoadhimishwa na kila Nchi Mwanachama wa Umoja huo kulingana na mazingira ya Nchi Husika.

Mhe. Senyamule amesema kwa mwaka huu maadhimisho haya yameanza rasmi tarehe 17 na kilele chake kitakuwa tarehe 20 mwezi Mei 2025 katika Viwanja vya Chinangali.

“ Wafugaji nyuki, wajasiriamali na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki na wadau wengine wa sekta ya Ufugaji Nyuki hukutana kwa lengo la kujengeana uwezo wa namna bora ya kuendeleza Sekta ya Nyuki katika Mkoa wa Dodoma na Nchi Yetu kwa ujumla.

Wadau wote wa sekta hii tunapaswa kuyatumia maadhimisho haya kikamilifu ili tuweze kujiinua kiuchumi na kuiendeleza Sekta ya Ufugaji Nyuki.

Mkoa wa Dodoma una zaidi ya mizinga 18,000 ya nyuki yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya kilo 135,000 za asali”Amesema  Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba,ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii amesema Nyuki amekuwa ni Muhimu sana kwenye maisha ya Mwanadamu, anastaili kuitwa kiumbe nyuki kwasababu ya kazi zake.

“ Umuhimu wa kiumbe huyu,  ametambuliwa siyo tu kwa binadamu hata kwenye maandiko ya vitabu vya Mungu yametaja sifa za kiumbe nyuki.Tunapojivunia maendeleo ya sekta ya nyuki  hatuna budi kutafakari kuhusu uendelevu wa sekta hii  kwa ujumla”amesema Wakulyamba.

Maadhimisho hayo yameenda sambaba  na kaulimbiu isemayo “Nyuki kwa Uhai na Uchumi Imara, tuwahifadhi’’.


#APIMONDIA 2027 Tanzania ipo tayari

#Dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.