• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI IMEJIPANGA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA ; WAZIRI GWAJIMA

Imetumwa : June 24th, 2025

Na; Happiness E. Chindiye

Habari - Dodoma RS

Serikali imejipanga vema kupambana na tatizo la dawa za kulevya kwa kuanzisha chombo mahsusi kijulikanacho kama Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), ambacho pamoja na majukumu mengine ina jukumu la kupunguza madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, kuratibu na kusimamia masuala ya tiba na huduma za utengamao kwa waraibu wa dawa za kulevya Nchini ikiwemo nyumba za upataji nafuu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Doroth Gwajima wakati la Kongamano la Vijana lililo andaliwa mahususi kwa ajili ya elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya lililofanyika ukumbi wa Mabele Jijini Dodoma.

“Mamlaka yetu ina jukumu la kutoa elimu sahihi kwa Umma juu ya athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya, kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya.

“Kwa hiyo tukio letu la leo linashabihiana kabisa na malengo na mikakati ya Serikali katika kuimarisha mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya. “ - Mhe. Gwajima

Hata Hivyo, Mhe. Gwajima amewasihi Vijana  kuwa mabalozi wazuri wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali dhidi ya tatizo la dawa za kulevya.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA), Bw. Aretas Lyimo amewaasa vijana kuachana na  Matumizi ya dawa za kulevya  kwani yanazima ndoto na kuweza kuwaingiza kwenye matokeo mabaya, ikiwa ni pamoja na uraibu, vitendo vya ukatili, matatizo ya kiafya kama vile UKIMWI, Magonjwa ya Akili, Kifua Kikuu pamoja na Homa ya Ini.

Kongamano hili ni mojawapo ya matukio yaliyopangwa kufanyika kuelekea Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita  Dawa za Kulevya Duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika Juni 26,2025 Jijini hapa.


&&&


#drugday2025

#wekezakwenyekinganatibadhidiyadawazakulevya

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.