• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI MBIONI KUJENGA BARABARA YA MPWAPWA - KONGWA - MBANDE KWA KIWANGO CHA LAMI

Imetumwa : June 23rd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, tayari imetoa fedha zinazohitajika kwa ajili ya  ujenzi wa Barabara ya Mpwapwa – Kongwa  - Mbande kwa kiwango cha lami, ili kumaliza kabisa kadhia wanayoipata wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma kutokana na matumizi ya barabara hiyo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, CPA Amos Makalla ameyasema hayo alipokua akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wakazi wa Wilaya hiyo na Wilaya jirani ya Kongwa Juni 23, 2025 katika eneo la Mnara wa Mashujaa Mpwapwa Sokoni.

“Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tayari ametoa fedha zote zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii ya Mpwapwa - Kongwa mpaka Mbande kwa kiwango cha lami. Mkandarasi tayari amepatikana na maandalizi ya ujenzi yanaendelea.

  Hatua hii ni ushahidi wa dhamira ya CCM na Serikali yake katika kuwaletea Maendeleo Wananchi”.

Aidha, ametaja mafanikio mengine yaliyotekekelezwa na Serikali katika Mkoa wa Dodoma chini ya Mhe. Rais Samia kuwa ni elimu bila malipo, ujenzi wa vituo vya afya, upatikanaji wa umeme vijijini pamoja na ujenzi wa madaraja, huku akisisitiza kuwa Serikali ya chama chake imeacha alama kwenye kila sekta Nchini.

Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Kibakwe na Waziri wa Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene ametaja maendeleo yaliyoletwa na Serikali kwenye Jimbo lake hususan ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo ile ya lami yenye urefu wa KM 3 ambayo haikuwahi kuwepo awali ikiwa na taa za barabarani na ujenzi wa KM 1 nyingine kukamilisha KM 4 unaendelea.

Jimbo la Kibakwe pekee limepatiwa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 3.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo kwenye sekta ya elimu wameongeza shule za msingi mpya 11 ambapo awali zilikua 65, shule za sekondari 10 mpya zikiwa na miundombinu yake ya maabara ambapo awali kulikua na shule 12 huku umeme ukifika kwenye vijiji vyote 113 vya Jimbo hilo.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.