• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SOKO LA MACHINGA DODOMA KUANZISHA DAWATI LA KIJINSIA KUPAMBANA NA UPOTEVU WA HAKI

Imetumwa : May 12th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ameelekezwa kuhakikisha kuwa soko la wafanyabiashara wadogo wadogo Jijini Dodoma maarufu kama ‘Machinga Complex’ linakuwa na dawati la jinsia ndani ya kituo kidogo cha Polisi kilichopo sokoni hapo ili kukabiliana na vitendo vya upotevu wa haki ya kijinsia.

Maelekezo hayo yametolewa Mei 12, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizindua rasmi Umoja wa Wanawake Machinga Dodoma (UWAMADO) katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya soko hilo Jijini Dodoma.

“Kama hapa kuna viashiria vya kupoteza haki ya kijinsia, hakikisheni leo tarehe 12, 05 hadi tarehe 30, Dawati la kijinsia liwe limeanzishwa hapa ili muweze kupata haki sawa. Nchi yetu haitaki kupendelea mtu mmoja, wanaume au wanawake, inataka wote wapate haki sawa, kituo cha Polisi tayari kipo hivyo, unao mwanzo wa kuanzia ili hili liweze kutokea”.

Akizungumza na wanawake hao pamoja na hadhira iliyojitokeza kushuhudia uzinduzi huo, Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Nishati Mhe. Anthony Mavunde amesema Jiji la Dodoma limetenga shilingi Bilioni 7 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa akina Mama, vijana na watu wenye ulemavu hivyo ameyataka makundi hayo kuchangamkia fedha hizo.

Nae, Meneja Msaidizi wa Soko la Machinga Bw. Mbwana Kasonta, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea soko hilo ambalo limepunguza adha ya kupigwa na jua pamoja na mvua mitaani hivyo limeongeza wateja wa kudumu sambamba na kuliweka Jiji katika hali ya usafi.

Awali, akisoma risala ya Umoja huo, Katibu wake Bi. Mariam Kajembe amesema, Umoja wao una ndoto ya kuanzisha SACCOS ili kupambana na ukosefu wa mitaji rafiki kwa ajili ya kufanyia biashara kwani wamekua wahanga wa kukosa mitaji ya kuendeshea biashara ambapo kuunga mkono hilo, zimetolewa shilingi Milioni 4 kuanzisha SACCOS hiyo.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NA DHAMIRA YA DHATI YA KILIMO CHA TUFAA (APPLE)

    May 12, 2025
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI ; WANANCHI WA WATAKIWA KUJITOKEZA

    May 12, 2025
  • SOKO LA MACHINGA DODOMA KUANZISHA DAWATI LA KIJINSIA KUPAMBANA NA UPOTEVU WA HAKI

    May 12, 2025
  • BILLIONI 14 KUJENGA OFISI ZA UBALOZI WA UGANDA JIJINI DODOMA

    May 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.