• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TANZANIA NCHI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUZALISHA TANI 34,000 ZA ASALI

Imetumwa : May 20th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Imeelezwa kuwa Tanzania inazalisha asali kiasi cha tani 34,000 na kuiweka katika ramani ya dunia kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kwa uzalishaji huo lakini pia inashika nafasi ya pili Barani Afrika.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) wakati akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya nyuki Duniani kilichofanyika leo Mei 20, 2025 kwenye viwanja vya Bustani ya Mapumziko Chinangali Jijini Dodoma.

“Kwa sasa Tanzania inazalisha tani 34,000 za asali. Kiwango hiki kinaiweka Tanzania katika ramani ya Dunia kwa kuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa asali kwa nchi za Afrika Mashariki, lakini pia katika Bara la Afrika, Tanzania ni nchi ya pili, kwenye hesabu ya Duniani, tumeshika nafasi ya 14 kati ya nchi zote”.

Kadhalika, Waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Pindi Channa, amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kutambua mchango wa mdudu nyuki na nafasi ya Tanzania katika maendeleo ya ufugaji nyuki Duniani hivyo wamefanya midahalo, semina na kutoa elimu kwa jamii juu ya uelewa wa siku hiyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mstaafu na mdau muhimu wa nyuki kwa Mkoa wa Dodoma Mhe. Mizengo Pinda ametoa ushauri kwa vijana kujihusisha na ufugaji nyuki ili kuinua kipato kupitia mazao yake pamoja na kuiusia jamii kuendelea kumuona mdudu huyo kama rafiki kutokana na msaada wake katika utunzaji wa misitu yetu.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Mkoa wake unaendelea kuhamasika katika ufugaji wa Nyuki kwa maslahi mapana ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

“Mkoa wa Dodoma umekua ni kati ya Mikoa inayohamasisha ufugaji wa nyuki, na inao wafugaji wa nyuki, lakini pia tunafurahi kuwa tuna viwanda vitatu ambavyo vinaendelea kuchakata mazao ya nyuki  na kuuza. Na tunamshukuru Mhe. Mizengo Pinda kwani shamba lake limekua ‘shamba darasa’ na kufanya Wanadodoma kuwa wafugaji wa Nyuki”.

Maadhimisho ya siku ya nyuki duniani ni utekelezaji wa Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa la tarehe 20 Desemba, 2017 ambalo lililenga kutambua mchango wa mdudu nyuki katika usalama na uhifadhi wa chakula na kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu 2025 ni “Nyuki kwa Uhai na Uchumi Imara, Tuwahifadhi”.


#APIMONDIA 2027 Tanzania ipo tayari

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.