• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI ; WANANCHI WA WATAKIWA KUJITOKEZA

Imetumwa : May 12th, 2025

Na; Happiness E. Chindiye

    Habari - Dodoma RS

Wananchi Mkoani hapa wamesisitizwa kujitokeza kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili utakaofanyika kuanzia tarehe 16  hadi 22 Mei, 2025 katika vituo vilivyo pangwa kwenye maeneo yao.

Hayo yameelezwa Leo tarehe 12 Mei,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule wakati alipokutana na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi yake,  Jengo la Mkapa Jijini Dodoma.

“Nawasihi wanadodoma wote wenye sifa wafike kwenye  vituo kuhakiki taarifa zao na kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na Tume huru ya uchaguzi “ - Amesema Mhe.Senyamule

Mhe. Senyamule amesema uboreshaji huo ni sehemu muhimu ya mchakato wa uchaguzi na unalenga kuhakikisha wapiga kura wote wanahakiki taarifa zao.

“Ni muhimu kwa wapiga kura kuhakikisha kuwa taarifa zilizopo kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ni sahihi ili waweze kutimiza haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025” - Amesisitiza

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo ameeleza  uboreshaji huo utafanyika katika Mkoa wote huu ambapo idadi ya vituo kwa Mkoa mzima ni 413, huku idadi kwa kila Halmashauri ikiwa kama ifuatavyo;Chemba vituo 58, Jiji la Dodoma vituo 105, Kongwa vituo 41, Mpwapwa vituo 67, Bahi vituo 32, Kondoa Vijijini Vituo 44, Kondoa Mji vituo 16 na Chamwino vituo 50.

Aidha, Vituo hivyo vitakuwa katika Ofisi za Watendaji wa Kata ambapo kwa kata ambazo ni kubwa, utaratibu umeshafanyika, vituo vimegawanywa,hivyo kutakuwa na vituo kwenye ofisi za kata na katika maeneo mengine ambayo Wananchi watatangaziwa   na Viongozi wao wa Kata, Mitaa/Vijiji.

Uboreshaji wa daftari awamu hii unahusisha kuandikisha wapiga kura wapya (wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawajajiandikisha, na watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025), kukagua daftari, Wapiga kura kuhakiki taarifa zao, Kufanya marekebisho ya taarifa pamoja na kuweka pingamizi kwa wapiga kura wasio na sifa kuendelea kuwemo kwenye daftari.


&&&


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NA DHAMIRA YA DHATI YA KILIMO CHA TUFAA (APPLE)

    May 12, 2025
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI ; WANANCHI WA WATAKIWA KUJITOKEZA

    May 12, 2025
  • SOKO LA MACHINGA DODOMA KUANZISHA DAWATI LA KIJINSIA KUPAMBANA NA UPOTEVU WA HAKI

    May 12, 2025
  • BILLIONI 14 KUJENGA OFISI ZA UBALOZI WA UGANDA JIJINI DODOMA

    May 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.