• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

" Uongozi wa Shule ya Sekondari Miyuji Mfano wa Kuigwa" RC -Mtaka

Imetumwa : July 8th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, leo ameupongeza uongozi wa shule ya Sekondari Miyuji kwa hatua yake ya kufunga CCTV kamera shuleni hapo kwa ajili ya usalama wa shule.

Mhe. Mtaka ameeleza kuwa Mkoa wa Dodoma una Shule za Sekondari 230 na shule za msingi 810, lakini kupata Mwalimu anayefikiria kufunga CCTV kamera Kwa ajili ya usalama wa Shule ni adhimu sana. Tungetamani kuona Shule zote zikiwa na kamera, kwani kumekuwa na matendo mengi ya kihalifu yakitokea maeneo ya shule.

 ‘’Mimi kama kiongozi, moja ya  kazi zangu ni kuwatambua watu wenye Uwezo na wanaofanya ubunifu,hivyo Mwalimu Mkuu nikupongeze sana kwa hatua hii nzuri uliyofanya. Umefanya kitu kizuri na ‘extraordinary’.Aidha nikupongeze kwa kuja na ubunifu wa kudhibiti utoro wa walimu ambapo walimu wa shule ya Miyuji badala ya kusaini kwenye daftari wakati wa kuja na kuondoka shuleni sasa watakuwa wanasaini kwa kutumia simu za mikononi/simu janja. Afisa Elimu Mkoa, watu wa aina hii ni mmoja wa watumishi bora kada ya elimu,hivyo ni vyema mkawatambua watu wa kaliba hii wakati wa sherehe za wafanyakazi bora. Kwani watu kama hawa baadae ndio wanatakiwa kuwa Maafisa Elimu, Wakurugenzi au hata baadae Makatibu Tawala”. Amesisitiza Mhe. Mtaka.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka walimu wa shule zote za mkoa wa Dodoma kuheshimu na kufanya kazi kwa kufuata,taratibu, kanuni na sheria. Kitu cha kwanza ni kazi yetu,kila mwalimu  aheshimu heshima aliyopewa. Walimu msifanye kazi kwa kuegemea nafasi ya mwenza wako na hivyo kukiuka taratibu za shule, hicho kitu hakikubaliki  kabisa Mkoani  Dodoma, mwalimu Mkuu, afisa Elimu Mkoa naomba nipate taarifa za walimu wenye tabia kama hizo ili washughulikiwe.

Akizungumza na wanafunzi, Mhe. Mtaka amewataka wanafunzi wote  zaidi ya 1300 wa shule ya Miyuji Sekondari kuzingatia masomo yao na rafiki wa kweli wa kike au wa kiume ni Shule yako. Mafanikio yako ndio mume au mke bora.

Jukumu la kumuelimisha Mwanafunzi na hatimae akafanya vizuri ni la Mzazi, Mwanafunzi mwenyewe na mwalimu, hivyo siku ya Jumanne 12/7/22 saa 10:00 jioni kila mwanafunzi aje na mzazi wake. Kwani ninataka kuzungumza na  Kila,mzazi mwenye mwanafunzi katika shule ya Sekondari Miyuji .

Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo kwa Afisa Elimu Mkoa, pamoja na walimu wa shule ya sekondari Miyuji Kuhusu namna bora ya kushughulika na wanafunzi wenye ufaulu hafifu, na kuwaahidi walimu kuwapatia zawadi  wanafunzi na walimu watakaofanya vizuri. Akizungumzia zawadi hizo Mhe. Mtaka  ameahidi kwa manafunzi yeyote toka shule ya sekondari ya Serkali akipata daraja la kwanza l la poini 7 ,mwanafunzi atapewa Tsh.500,000/-  kama zawadi. Kwa Walimu kila  A @ 30,000/- na kila B@ 5000/-. Kwa Wasichana wote watakaopata 1 ya tarakimu moja pamoja na zadi ya fedha mwanafunzi huyo atapatiwa uniform za shule, Wanafunzi wenye ulemavu watakao pata daraja la kwanza na la pili watapatiwa  mahitaji yote  ya shule.

Akizungumza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Miyuji Mwl. Greyson Maige,ameeleza kuwa shule hiyo ya sekondari ilianza mwaka 2006 na ina jumla ya wanafunzi 1346.Mwl.Maige alieleza mikakati amabyo shule yake imejiwekea ili kuinua ufaulu ambayo ni pamoja na kuhakikisha kwamba inamaliza mada za kidato cha nne kufikia mwezi macho jambao amablo wamefanikiwa .Kufundisha kwa umoja,kukutana na wazazi na hatimae kuwaeleza mkakati wa shule ilikuinua ufaulu,kufanya mitihani ya mara kwa mara, walimu kugawiwa wanafunzi wafiofanya vibaya ili kuwafanyia uangalizi wa karibu zaidi.

Aidha Pamoja na mikakati hiyo Mkuu wa Shule ameeleza kuwa Shule ya sekondari Miyuji inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile upungufu wa Walimu wa Sayansi na hisabati ,mwamko wa wazazi hasa kwa wanafunzi wenye ufaulu hafifu,shule kukosa uzio, upungufu wa vitabu, shule kuwa katikati ya makazi ya watu, uhaba wa viti na meza kwa walimu na wanafunzi,ukosefu wa jingo la uatawala na maktaba, ukosefu wa viwanja  na vifaa vya michezo,kukosekana kwa nyumba za wlimu na ukumbi a shule pamoja na ukosefu wa vitabu vya masomo ya biashara, physical education na fizikia.

Mwl. Maige amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea shule ya sekondari Miyuji, aidha amewashukuru sana walimu wenzake kwa ushirikiano wanaompa katika suala zima la ufundidhaji na malezi ya wanafunzi kwa ujumla.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

    May 18, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.