• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

USALAMA BARABARANI WATAKIWA KUWA JAMBO LA KIMKAKATI KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI

Imetumwa : June 19th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Imeelezwa kuwa jukumu la usalama barabarani linapaswa kuwa la pamoja na la kimkakati ili kupunguza madhara yanayotokana na ajali za barabarani. Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya alipokua akifungua kikao chechemuzi kuhusu Mradi wa Usalama Barabarani kwa Jamii-Mkuza wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP).

Kikao hicho kimefanyika leo Juni 19, 2025 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Vizano Jijini Dodoma, kikiangazia mambo kadha wa kadha yanayohusu Usalama Barabarani kwenye barabara zilizopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo kwa Mkoa wa Dodoma limepita kwenye Wilaya za Chemba na Kondoa.

“Inaonesha dhahiri kuwa, jukumu la usalama barabarani linapaswa kuwa la pamoja na linalohitaji Mkakati kamili na ubunifu wa hali ya juu kupunguza madhara yanayotokana na ajali za barabarani, hivyo ni muhimu kwa ushuhuda wa dhati na dhamira yetu ya kukuza na kujenga miundombinu sahihi kwa jamii yetu kwani inaacha alama endelevu juu ya elimu ya usalama barabarani”.  Bw. Mmuya.

Aidha, Mratibu wa Usalama Barabarani kutoka Shirika la AMEND kwenye Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Bi. Suzana Hamaro ameeleza kuwa, kipengele kikuu cha Mradi ni shughuli za usalama barabarani kwa ngazi ya jamii ambapo wanatoa elimu ya usalama barabarani shule za msingi na sekondari sambamba na kuangalia makundi hatarishi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Tamim Songoro, amesema Jeshi lake linashirikiana na AMEND kutoa elimu juu ya usalama wa barabarani hasa kwa watembea kwa miguu ambao ndio wahanga wakubwa wa ajali za barabarani kwa kutofahamu sheria za usalama barabarani.

AMEND ni Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na utoaji wa elimu ya usalama barabarani likifanya kazi katika nchi zaidi ya 10 Barani Afrika, kwa lengo la kuboresha hali ya usalama barabarani, kwani jambo hilo ni janga la Kimataifa. Nchini Tanzania Mradi huo umepita kwenye Mikoa 8 ikiwemo Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.