• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WABUNGE WAHAMASISHWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI

Imetumwa : June 21st, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wadau mbalimbali wa michezo, wamehamasishwa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya mwili kwani yana umuhimu mkubwa si tu kwa afya bali hata kimahusiano baina yao, sambamba na kuongeza ufanisi kiutendaji.

Hamasa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokua akiwahutubia Wabunge na wadau hao baada ya kutamatika kwa michezo iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa jina la ‘Bunge Grande Bonanza’ ambayo hufanyika kila mwaka, na mwaka huu limefanyika Juni 21, 2025 kwenye Viwanja vya Shule ya St. John Merlin Jijini Dodoma.

“Mazoezi haya tuliyoyafanya kupitia michezo hii na kupitia ‘Bunge Bonanza’ yana umuhimu mkubwa, si   tu kwa afya bali pia yanajenga urafiki miongoni mwetu, mahusiano mema miongoni mwetu ya kimichezo, lakini pia inaimarisha afya ya akili hivyo kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu yetu ya kila siku katika maeneo yetu.”

Aidha, akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spika Mhe. Azzan Zungu, amesema Bonanza hili ni la mwisho kwa kipindi hiki ambacho Bunge linavunjwa na kwenda kwenye mchakato wa uchaguzi hivyo, amewashukuru Wadau wote waliohusika kwenye maandalizi ya shughuli hiyo.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepata fursa ya kutoa salam za Mkoa ambapo amewashukuru Wabunge wote kwa ushirikiano wao na Mkoa na kuwaambia kuwa wao ni jamii moja ya Mkoa wa Dodoma.

“Wabunge hawa ni wenzetu, rafiki na ndugu zetu lakini pia tunafanya nao biashara hivyo wao ni sehemu ya jamii ya Dodoma. Kama tunavyofahamu Mhimili wa Bunge ulikuwepo muda mrefu hapa Dodoma na katika awamu hii tumebahatika kupokea Mihimili miwili ya nchi hii lakini wao wakiwa ni waanzilishi”.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bw. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema, Benki yake inafanya mambo ya kijamii ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwani ndio utaratibu waliojiwekea kusaidia watu waliofikwa na majanga mbalimbali sambamba na kuandaa mabonanza ya michezo.

Katika hatua nyingine, Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya  Bw. Aretas Lymo, amesema wameshirikiana na Benki ya CRDB kuandaa Bonanza hilo kuelekea Maadhimisho ya siku ya Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani kwani dawa hizo ni uhalifu wa kupangwa unaoharibu uchumi, ustawi wa jamii pamoja na vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.

Benki ya CRDB imekua na utaratibu wa kudhamini Mabonanza ya michezo maarufu kama ‘Bunge Grande Bonanza’ kwa tangu mwaka 2021 ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka katika mwezi Juni katikati ya Bunge la Bajeti ambapo mwaka huu lilianza kwa matembezi kutoka Chuo cha Mipango kuelekea Viwanja vya St. John Merlin na kupambwa na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kikapu, kukimbiza Kuku na mingine mingi.


 #drugday2025

#wekezakwenyekinganatibadhidiyadawazakulevya

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.