• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAMILIKI WA VITUO VYA KULELEA WATOTO WADOGO MCHANA WAHIMIZWA KUVISAJILI KUEPUSHA WATU WASIO SAHIHI

Imetumwa : June 21st, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA

Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo  Mchana, wametakiwa kuvisajili  vituo hivyo, ili kuepusha hatari ya kutokuwa na watu sahihi katika eneo la  malezi na Makuzi ya watoto.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya katika kikao cha kujadili utoaji wa huduma ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika vituo vya kulelea watoto wadogo mchana kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jijini hapa Juni 21, 2025 kikiwahusisha wamiliki wa vituo hivyo.

“Ninasikitika kuwa katika vituo 243, vituo 167 havijasajiliwa, maana yake inawezekana havijakidhi vigezo, na kitu kimoja kikubwa ninachokiogopa ni kuwa na watu wasio sahihi katika eneo la makuzi na malezi, kulea watoto katika mfumo huu ambao Serikali imeweka ni kazi kabisa anasomea mtu”. Bw. Mmuya.

Aidha, Bw. Mmuya amesisitiza kuwa Mkoa hautafurahia kuwa na vituo ambavyo havijasajiliwa, hivyo amewataka Wamiliki wa Vituo hivyo ambavyo havijasajiliwa, kujitafakari baada ya kikao hicho kwa kukubaliana muda, na kama kutakua na changamoto yeyote wasisite kuwasiliana na Msajili ili awasaidie kupita kwenye hatua za usajili.

Awali, akiwasilisha changamoto katika uanzishwaji na uendeshwaji wa vituo hivyo, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Josephine Mwaipopo, ametaja moja ya changamoto kuwa ni uwepo wa vituo vilivyoanzishwa kiholela ambavyo mazingira yake ni hatarishi kwa maisha ya watoto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa mazingira rafiki.

Naye, Mwenyekiti wa wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo Mchana Mkoa wa Dodoma Bi. Rehema Mdengede, amesema watu wengi wamekua wakianzisha na kuendesha vituo hivyo bila kufuata kanuni na taratibu,  hali iliyosababisha kutokea kwa matukio ya kikatili wanayofanyiwa watoto kwenye baadhi ya vituo hivyo.

Vituo vya kulelea Watoto Wadogo Mchana vimeanzishwa kwa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009 iliyofanyiwa mapitio 2019 pamoja na Kanuni ya uanzishaji na uendeshaji wa Vituo hivyo ya mwaka 2020 inayosema “mahali palipoandaliwa kwa ajili ya malezi wakati wa mchana kwa watoto wenye umri usiozidi miaka mitano na usiopungua miwili” na huanzishwa na kuendeshwa na watu binafsi, taasisi zilizosajiliwa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Mashirika ya Dini pamoja na Taasisi za Serikali.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.