• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WA DODOMA KUSIKIA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KILA KATA (SAMIA DAY)

Imetumwa : June 2nd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma unatajwa kufaidika zaidi na Miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo ya Kimkakati, Maendeleo na ile yenye manufaaya ya moja kwa moja kwa wananchi ambayo imetekelezwa katika ngazi  ya Kata hivyo, Uongozi wa Mkoa umeandaa ‘Dodoma Samia Day’ ili wananchi wapate fursa ya kusikia na kuyasema yale yaliyofanyika katika Kata zao.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amebainisha hayo wakati wa Mkutano na Waaandishi wa Habari kwenye ukumbi wa ofisi yake Jijini humu kuzungumzia tukio hilo leo June 02, 2025 ambapo tukio hilo linatarajiwa kufanyika June 03.

“Sisi Mkoa wa Dodoma katika kipindi cha awamu ya sita, tumepokea miradi ambayo imegharimu zaidi ya shilingi Trilioni 10 ya fedha za Kitanzania. Miradi hiyo ni ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa nje KM. 112.3 unaogharimu shilingi Bilioni 221, ujenzi wa barabara ya Ntyuka –Mvumi-Kikombo KM 25 kwa shilingi Bilioni 25”.

Aidha, baadhi ya miradi aliyoitaja ni pamoja na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kutoka Megawati 48 mwaka 2020/21 hadi megawati 200 kwa gharama ya shilingi Bilioni 53. Ujenzi wa Mradi wa umeme Zuzu wenye uwezo wa kupooza umeme megawati 32 hadi megawati 200 kwa gharama ya shilingi Bilioni 202.

Mbali na hilo, Mkuu wa Mkoa amesema pamoja na miradi hiyo iliyotekelezwa katika ngazi ya Mkoa (miradi mikubwa ya kimkakati) lakini, ipo miradi iliyotekelezwa kwa ngazi ya Halmashauri, ametaja gharama za miradi hiyo kwa ujumla wake kwa kila Halmashauri ambapo katika Halmashauri ya Bahi, Miradi yenye thamani ya Bilioni 23.9 imetekelezwa.

“Chamwino imetekeleza miradi ya shilingi Bilioni 99.8, Chemba Miradi ya Bilioni 24.1, Jiji la Dodoma miradi ya shilingi Bilioni 151.4, Kondoa miradi ya Bilioni 23.2, Kondoa Mji miradi ya Bilioni 12.4, Kongwa miradi ya Bilioni 55.9 na Mpwapwa miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 77.2” Mhe. Senyamule.

Sanjari na hayo, Mhe. Senyamule ameongeza kuwa, kila Kata imejiandaa kusherehekea siku hiyo kwa namna yake kwani zipo ambazo zimeanzisha mashindano ya michezo mbalimbali ambapo tarehe June 03, 2025, itakua fainali, kadhalika, kutakuwa na uwasilishaji wa taarifa za mafanikio ya Serikali pamoja na burudani kutoka kwa wasanii na vikundi mbalimbali vya Sanaa vilivyopo katika maeneo yao.


#dodomatumetekeleza,kaziinaendelea

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAS MMUYA AWAAHIDI ZAWADI NONO WANAMICHEZO - UMITASHUMTA

    June 17, 2025
  • WAMILIKI WA MAABARA BINAFSI WATAKIWA KUTOA MAJIBU SAHIHI YA VIPIMO KWA WAGONJWA

    June 17, 2025
  • TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUJIUNGA NA MFUMO KURAHISISHA HUDUMA KWA WANANCHI

    June 17, 2025
  • DODOMA MOTO MKALI MASHINDANO UMITASHUMTA

    June 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.