• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WAHAMASISHWA KUPINGA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Imetumwa : June 20th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wananchi wamehamasishwa kupinga matumizi ya Dawa za Kulevya kwani zina athari kubwa kwenye mifumo ya fahamu ya binadamu. Hamasa hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Daktari Thomas Rutachunzibwa wakati wa zoezi la usafi wa mazingira ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma leo Juni 20, 2025.

Zoezi hilo la usafi limeandaliwa kwa lengo la kutoa hamasa kwa Wananchi, kuelekea kilele cha maadhimisho ya  Siku ya Kupiga vita dawa za kulevya Duniani ambayo huadhimishwa Juni 26,kila mwaka ili waweze kushiriki maadhimisho hayo yatakayofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

“Kabla ya siku yenyewe, zimepangwa shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na zoezi hili la leo, ambapo kupitia shughuli hizo tunatoa jumbe za kuhamasisha jamii kutotumia dawa za kulevya lakini wale ambao wametumia dawa hizo, waelimishwe namna gani ya kupata matibabu ili waweze kuondokana na hilo tatizo”.

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Kamishna wa Kanda ya Kati Bw. Joseph P. Kisusi amesema Mpango wa matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya unasaidia kupunguza madhara ya dawa hizo kwa wale ambao tayari wameathirika kwani kwa sasa wengi wanajitokeza kutokana na juhudi za Serikali kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo Nchini.

Aidha baadhi ya wananchi  walioshiriki zoezi hilo la usafi , wameipongeza Serikali kwa juhudi hizo kwani matumizi ya dawa za kulevya yanaharibu vijana ambapo wengi walioathirika hugeuka kuwa mzigo kwa wazazi.Sambamba na pongezi, wameiomba Serikali kuendelea na mapambano dhidi ya mianya ya dawa hizo kuingia au kuzalishwa, ili kuwa na kizazi imara siku za usoni.

Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani 2025 yanaambatana na shughuli mbalimbali zilizoandaliwa na Mamlaka yenye dhamana kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,ikiwa ni pamoja na mabonanza ya michezo, kushiriki usafi kwenye maeneo ya kijamii na kutoa elimu kwa makundi ya mitaani pia kupitia vyombo vya habari juu ya athari za  dawa hizo.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.