• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE WAASWA KUSIMAMA KATIKA NAFASI ZAO

Imetumwa : March 4th, 2023

Umoja wa Wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma hii leo tarehe 3 Machi 2023 umeadhimisha Kongamamo na ibaada ya maombi ya wanawake dunia nzima iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,  Dayosisi ya Dodoma na katika Viwanja vya Kanisa Katoliki Kongwa.

Akifungua kongamano hilo la maombi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema wanawake ni nguzo katika jamii na chachu ya maendeleo hivyo ni muhimu kwa kundi hili kusimama katika nafasi zao katika kuliombea Taifa, Kanisa na familia ili kuwa kizazi chenye maadili, uzalendo na hofu ya Mungu.

Aidha, Senyamule amewakumbusha jukumu lao kama wanawake na walezi kwa kusisitiza kuwa kila mmoja ana mchango mkubwa katika kufanikisha ustawi katika ngazi ya jamii. “Kumekuwa na  mmonyoko wa maadili katika jamii zetu, kila mmoja ana mchango katika kusimamia maadili na makuzi ya vijana huku tukikemea kwa dhati suala la ukatili wa kijinsia ” alisisitiza Mhe. Senyamule.

Amewataka akina mama hao kuwa na moyo wa kujiamini, kuthubutu na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia miradi ya maendeleo na kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali.

Serikali imefanya makubwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na changamoto za uzazi. Amesema Serikali imetoa kipaumbele katika ujenzi wa Hospitali, Zahanati na ununuzi wa Vifaa na vifaa tiba katika kuimarisha sekta ya afya nchini.

Akizungumzia elimu Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma umepiga hatua kubwa katika kuimarisha miundombinu ya elimu kwa kukamilisha ujenzi wa madarasa, vituo shikizi na upatikanaji wa madawati kwa wanafunzi

“Mkoa wa Dodoma tumependelewa katika sekta ya elimu kuna Shule za kutosha, Vyuo vya kati na vile Vikuu, kazi iliyobaki ni kwetu wazazi kuhakikisha watoto wetu wanaenda shule, Serikali imetimiza wajibu wake, na sisi wazazi tutumize wajibu wetu” Amesisitiza Mhe. Senyamule.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga ametoa rai kwa wanawake wa Dodoma kuwa na malengo mahsusi katika maombi yao ambayo kwayo watajipima mwaka ujao.

“Tuchague mambo ya kuombea na mwaka ujao tuje hapa na shuhuda tukimshukuru Mungu kwa kufanikisha. Tusimame katika nafasi zetu ili tuweze kufanikiwa pia katika kukuza uchumi kwa maendeleo endelevu” Alisisitiza Dkt. Mganga.

Katika kuadhimisha siku hiyo ya maombi, Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kongwa umetoa vyakula na zawadi mbalimbali kwa wahitaji. Umoja wa Wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma unaundwa na akina mama kutoka makanisa ya KKKT, Roman Catholics, Anglikana, Moravian na TAC.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

    May 18, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.