• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"WAWEKEZAJI JITOKEZENI KUWEKEZA JIJI LA DODOMA"RC SENYAMULE

Imetumwa : October 1st, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea miradi mitatu iliyoanzishwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambayo ni City Hotel, Stendi kuu ya Mabasi Nanenane na soko la Job Ndugai.

Lengo la kutembelea miradi hiyo ni kukagua maendeleo yake na kuangalia kama lengo la kuanzishwa kwa miradi hiyo linatekelezwa kwani kuna baadhi ya miradi imekamilika lakini haifanyi kazi kama ilivyokusudiwa.

 “Kutokufanya kazi kwa miradi iliyoanzishwa kwa kodi za wananchi, ni kuwakosea wananchi kwani ni mali yao.Majengo mengi ambayo yamejengwa ndani ya miradi kwa lengo la uwekezaji, bado hayafanyiwi kazi ikiwemo soko kuu la Job Ndugai, stedi kuu ya mabasi Nanenane nafasi zipo ila wawekezaji hakuna. Natoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kwa wingi ili maeneo yote yafanyiwe kazi kama matarajio yaliopo” Amesema Senyamule.

``Serikali ilitarajia kupata mapato mengi kutokana na miradi hii lakini hali imekua tofauti kwani mapato ya sasa hayana uwiano na ukubwa wa miradi, kuna mambo madogo madogo kama utunzaji wa mazingira ni muhimu kwani kipo ndani ya uwezo wetu na ni suala la kupanga watu kuweza kuweka mazingira safi kulingana na hadhi ya eneo”  Amesisitiza Mhe Senyamule.

 Aidha,Mkuu wa Mkoa amehimiza uhamasishaji kwa njia ya matangazo hasa sehemu zilizo wazi kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kwani kuna kumbi kubwa na zinazofaa kwa ajili ya kufanyia mikutano na shughuli mbalimbali na zipo eneo zuri la mjini. Pia kuna maduka ambayo bado hayajapata wawekezaji na wanatakiwa kuja haraka kwani hii itasaidia kupata mapato ambayo yataboresha huduma za jamii.

Hata hivyo, Kaimu Mchumi wa Jiji la Dodoma Bw. Amani Ng’oma ameongozana na Mkuu wa Mkoa kwenye ziara hiyo, amezungumzia suala la madereva wa stendi kuu ya nanenane ambao hawaitumii stendi hiyo jambo ambalo linapoteza lengo la uwepo wake.

``Tunaomba msaada wako Mkuu wa Mkoa hasa kwa madereva wa mabasi makubwa ya abiria wanaokwenda au kuingia kutoka mikoa mbalimbali waweze kufuata utaratibu uliopo katika stedi hii kwani itapunguza changamoto ambazo zinazojitokeza kwa wananchi kwa kuwa kituo hiki kimejengwa kwa ajili yao na kwa fedha nyingi lakini wao wanakiuka taratibu za upakiaji na ushushaji abiria ndani ya kituo kwani usalama wao upo ndani kituo hiki``amesema Ng`oma.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

    May 18, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.