• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SUALA LA AMANI SI LA KISERIKALI TU BALI NI LA KIIMANI KUPITIA VITABU VITUKUFU

Imetumwa : October 26th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Suala la Amani na mshikamano limeendelea kuwa ajenda kuu ya Mkoa wa Dodoma hasa kwa makundi ya Madhehebu ya Dini ambapo inasemekana kuwa suala hilo si la Kiserikali bali ni la Kiimani bila kujali itikadi za Dini, ambalo limejidhihirisha kupitia vitabu vitukufu vya Mwenyezi Mungu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa hafla ya Maulid ya kumbukizi ya Mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) iliyokwenda sambamba na Dua maalum ya kuliombea Taifa zikiwa zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi Mkuu, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) kwenye viwanja vya Msikiti wa Gaddafi Jijini Dodoma Oktoba 26, 2025.

“Wanawake tunasema Tanzania tunaomba umoja, wa Kitaifa, tunaomba mshikamano, tunaomba watu wapatane, sisi ni wamoja haijalishi Dini zetu, makabila, vyama vyetu vya siasa. Lakini leo pia kitabu hiki cha Mwenyezi Mungu kinatuambia maneno haya haya ya upatanisho, niwaombe wanawake wa JUWAKITA tuwe mbele, tuwaambie wengine maneno haya kwani si ya Serikali bali ya kiimani”,

Aidha, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Bi. Pili Mbanga, amewasisitiza Wanawake  hao kuungana kuombea amani kwani wao pamoja na watoto,ndio waathirika wakubwa  pindi inapotoweka,huku akiwaomba kukaa na vijana majumbani na kuzungumza nao wasirubuniwe na maneno ya mitandaoni yanayohamasisha uvunjifu wa amani.

Vilevile, Mlezi wa JUWAKITA Kanda ya Kati Bi. Fatma Msindi, amesema kabla ya kuzungumzia amani kwa ujumla, amani kubwa ni ile ya nafsi ya mtu kuhakikisha ipo salama na kuongeza kuwa, amani haiwezi kupatikana kwenye nafsi ya mtu kama mtu huyo hajajitambua, kubadilika na kuacha mazoea.

Akitoa shukrani kwa Mgeni rasmi, Mwenyekiti Mtawala wa JUWAKITA Mkoa wa Dodoma Bi. Aisha Mjegere ametoa witi kwa kila mwanamke atakayetoka hapo kwenda na kauli ya Viongozi hao ambayo ni kudumisha amani, kwani inapokosekana anayeathirika ni mwanamke hivyo, amewataka kuheshimu walichopewa na Mwenyezi Mungu.

#DodomaFahariyaWatanzania

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigakura

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • STAKABADHI GHALANI KURAHISISHA BIASHARA KWA MFUMO WA HAKI NA UWAZI

    October 25, 2025
  • SUALA LA AMANI SI LA KISERIKALI TU BALI NI LA KIIMANI KUPITIA VITABU VITUKUFU

    October 26, 2025
  • WAHITIMU WA ELIMU YA JUU WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO DODOMA

    October 23, 2025
  • WANANCHI WASISITIZWA KUTUMIA HUDUMA ZA AFYA NA KUACHANA NA ZILE ZA KIENYEJI

    October 23, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.