• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WASISITIZWA KUTUMIA HUDUMA ZA AFYA NA KUACHANA NA ZILE ZA KIENYEJI

Imetumwa : October 23rd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Jamii imesisitizwa kutumia huduma za Afya zilizowekezwa na Serikali kwa kufika Hospitali mapema pindi wanapopata matatizo ya kiafya na si kukimbilia tiba za kienyeji kwani huduma zinapatikana kwa aina tofauti tofauti ikiwemo zile za Kibingwa na  Bobebu sambamba na uwepo wa Wataalam wa kutosha kwenye vituo vya ngazi zote.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo alipomtembelea Mtoto Bisadya Iddi mwenye umri wa Miaka 11 Oktoba 23, 2025, aliyepata ajali ya kuungua kwa moto kwenye baadhi ya maeneo ya mwili takribani mwaka mmoja uliopita na kwa sasa anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

“Huduma za afya zipo nyingi za kitaalam na karibu na sisi, wataalam wa afya wapo wakutosha kuanzia Madaktari wa kawaida, Bingwa na Mabingwa Bobezi, katika Mkoa huu hakuna ngazi ambayo unaweza kuikosa lakini pia vifaa vipo vya aina mbalimbali pamoja na dawa. Inasikitisha kuona bado kuna wananchi wanapata matatizo na hawatumii huduma hizo ambazo zipo rafiki kwa ajili yao.

Nitoe wito kwa wananchi wa Kondoa na Dodoma kwa ujumla kuwa zipo huduma za Afya, Mhe. Rais amewekeza sana katika sekta ya Afya. Leo tunazungumzia mtu aliyeungua akakaa mwaka mmoja bila kuletwa kwenye vituo vya afya akitumia huduma za kienyeji zikamchelewesha sasa mguu ule haunyooki”. Mhe. Senyamule.

Akizungumzia maendeleo ya Mtoto huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kondoa Bw. Shaaban Millao, amesema walichukua uamuzi wa kumchukua kutoka kwa wazazi wake na kumpeleka Hospitalini hapo na sasa anaendelea vizuri na matibabu huku akisubiriwa apone vidonda ili apate huduma ya kunyooshwa mguu wake na kurejea katika hali ya kawaida.

Nae, Baba wa Bisadya Bw. Iddi Bakari, ameishukuru Serikali kwa msaada walioutoa kuokoa maisha ya Mtoto wake huku akitoa wito kwa wananchi wenzake kutojitibu kienyeji pindi wanapopata matatizo ya kiafya bali wakimbilie huduma kwenye vituo vya Afya kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali kwani kupitia Mtoto wake, amepata funzo kubwa.

Licha ya kumtembelea Mtoto huyo, Mhe. Senyamule amekagua mradi wa ujenzi wa majengo katika Hospitali hiyo ambayo ni majengo ya Upasuaji, Wodi ya Upasuaji ya Wanaume, Wodi ya Upasuaji ya Wanawake, umaliziaji wa Bohari ya Dawa na umaliziaji wa jengo la utawala, yote yakigharimu shilingi 811,988,120.50 na Mradi unaendelea kwa hatua za umaliziaji.

Aidha, Mhe. Senyamule ametembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, matundu 12 ya vyoo vya Elimu msingi, vyumba viwili vya madarasa na matundu 6 ya vyoo kwa ajili ya elimu ya awali ukigharimu shilingi Milioni 131 kupitia Mpango wa BOOST kwenye shule ya msingi Iboni, mradi unaolenga kupunguza uchakavu wa miundombinu inayotokana na ukongwe wa shule sanjari na kuboresha mazingira ya kujifunzia.


#DodomaFahariyaWatanzania

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigakura

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAHITIMU WA ELIMU YA JUU WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO DODOMA

    October 23, 2025
  • WANANCHI WASISITIZWA KUTUMIA HUDUMA ZA AFYA NA KUACHANA NA ZILE ZA KIENYEJI

    October 23, 2025
  • KILA ALIYE TUMIA MUDA WAKE KUJIANDIKISHA AKAPIGE KURA

    October 21, 2025
  • MALEZI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM/WALEMAVU NI JUKUMU LA JAMII NZIMA

    October 21, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.