• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAHITIMU WA ELIMU YA JUU WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO DODOMA

Imetumwa : October 23rd, 2025

Na Bilali A. Juma

   Habari - DODOMA RS

Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Dodoma pamoja na Wahitimu waliokuwa Viongozi wa Serikali za Wanafunzi katika Vyuo hiyo,wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ofisini kwake,jengo la Mkapa Jijini Dodoma Oktoba 22, 2025.

Lengo la ziara ya Vijana  hao ni kujitambulisha  kwa Mkuu wa Mkoa,kueleza shughuli wanazozifanya,malengo waliyonayo kwa siku za usoni,sambamba na kutaka kufahamu fursa zilizopo,ambazo wanaweza kuzitumia kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.

Akizungumza na Vijana hao Mhe. Senyamule amesema kuwa mazingira ambayo yametengenezwa,yameifanya Dodoma kuwa Mji wa kipekee na wakuvutia,wenye  fursa,wenye amani,wenye mambo mengi mazuri.Na kwamba anafurahi kuona kuwa  wameshaanza kuziona fursa hizo.

"Lakini pia ukiijua mipango ya Dodoma utaona kuwa Dodoma inatarajiwa kuwa Mji mzuri sana Tanzania,na  huenda ikawa sio Tanzania tu,hata  Afrika.Utakuja kuwa mji wa kipekee kutokana na mipango iliyopo.Tunayaona machache; Mji wa Serikali ni wa kipekee,mahakama ni ya kipekee,barabara ya mzunguko ni ya kipekee,Ikulu iko hapa.

Kwa hiyo yako mambo ambayo yameanza kuonekana ya kipekee.Lakini ukisikia mipango inayokuja; treni ya 'local motive' barabara zetu zitatanuliwa kwenda airport,SGR,nyie ni  Wanavyuo mtakuwa mnafahamu kuwa Chuo kikubwa kabisa Afrika cha IT  kinaanza kujengwa pale Nala,na ramani wameshatutolea,sasa hivi wanatuonyesha kuwa mwaka huu imeshaanza kuwekwa kwenye bajeti.Kwa hiyo ukiiona Dodoma unaona kabisa kwamba ni mahali penye fursa nyingi"Amesema Mhe. Senyamule.

Aidha Mhe. Senyamule amewaasa vijana hao kuwa waaminifu kwani ,uaminifu ni kitu ambacho vijana wengi wa sasa hawana,hali inayowasabisha kukosa fursa nyingi kutokana na kutokuaminiwa.

Vijana hao ambao wametoka vyuo mbalimbali vilivyopo Dodoma wamepata nafasi ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa na kuelezwa juu ya fursa zilizopo.

Miongoni mwa fursa walizoelezwa ni zile zilizopo katika sekta ya Utalii, ambapo wameaswa kuwa mstari wa mbele kuzijua na kuzichangamkia,  ili wasikae mitaani na kuilaumu Serikali kuhusu ajira.

#DodomaFahariyaWatanzania

#KeroYakoWajibuWangu

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigaKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAHITIMU WA ELIMU YA JUU WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO DODOMA

    October 23, 2025
  • WANANCHI WASISITIZWA KUTUMIA HUDUMA ZA AFYA NA KUACHANA NA ZILE ZA KIENYEJI

    October 23, 2025
  • KILA ALIYE TUMIA MUDA WAKE KUJIANDIKISHA AKAPIGE KURA

    October 21, 2025
  • MALEZI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM/WALEMAVU NI JUKUMU LA JAMII NZIMA

    October 21, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.