• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUANZA UJENZI SHULE YA SEKONDARI LOJE

Imetumwa : October 27th, 2025

•Itaanza kutumika Januari 2026

• Wazazi wasema,itawaondolea watoto wao adha ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu ya  Sekondari Vijiji Jirani.

Na: Elizabeth Dai

Habari Dodoma Rs

Serikali imeahidi kuchukua hatua za haraka kuhakikisha changamoto ya kukosekana  kwa shule ya Sekondari katika kijiji cha Loje, wilayani Chamwino, inatatuliwa mara moja kupitia ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika eneo hilo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora katika sekta zote muhimu, ikiwemo elimu.

“Serikali inakusudia kuhakikisha inawaletea wananchi wake maisha bora katika sekta zote. Sasa nimesikia kuna changamoto ndogo ya elimu wananchi wa Loje mnayo, nimekuja hapa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kuwahakikishia kwamba Serikali ipo pamoja nanyi,” alisema Dkt. Kazungu.

Dkt. Kazungu aliongeza kuwa Serikali imeamua kuharakisha mchakato wa ujenzi wa shule hiyo ili wanafunzi wa eneo hilo waanze masomo mapema iwezekanavyo katika shule hiyo.

“Nitumie nafasi hii kuwahakikishia kuwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Loje unaanza mara moja. Iwe jua, iwe mvua, ujenzi unaanza haraka sana,” alisisitiza Dkt. Kazungu

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino, Bw. Tito Mganwa, alisema maelekezo ya Serikali ni kuhakikisha shule hiyo inakamilika kwa muda mfupi ili iweze kupokea wanafunzi mwezi Januari mwakani.

“Maelekezo ya Serikali ni kwamba sekondari hii mwezi wa kwanza inapokea wanafunzi. Kazi yangu ni kuratibu, kazi yenu ni kutoa ushirikiano, na tunaanza leo kwa kufanya usafi wa mazingira ili wataalam wanapokuja 'kuseti' ramani wakute pako safi,” alisema Bw. Mganwa.

Aidha, imebainika kuwa kata ya Loje imetenga jumla ya hekari 24.6 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo, hatua inayothibitisha ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na Serikali katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa elimu.

Wananchi wa Loje wamepokea kwa furaha hatua hiyo ya Serikali, wakisema shule hiyo itasaidia kupunguza changamoto ya watoto wao kutembea umbali mrefu kufuata elimu ya sekondari katika vijiji vya jirani na kuipa thamani kata hiyo iliyoanzishwa kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Ujenzi wa Shule ya Sekondari Loje unatarajiwa kuanza rasmi ndani ya siku chache zijazo, ukiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuboresha miundombinu ya elimu katika maeneo ya vijijini Nchini.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI KUANZA UJENZI SHULE YA SEKONDARI LOJE

    October 27, 2025
  • MKOA UTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA KINGA NA UDHIBITI WA MAJANGA YA MOTO

    October 27, 2025
  • STAKABADHI GHALANI KURAHISISHA BIASHARA KWA MFUMO WA HAKI NA UWAZI

    October 25, 2025
  • SUALA LA AMANI SI LA KISERIKALI TU BALI NI LA KIIMANI KUPITIA VITABU VITUKUFU

    October 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.