• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

CCTV CAMERA KUFICHUA WAVUNJIFU WA SHERIA KATIKA JIJI LA DODOMA

Imetumwa : September 30th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wito umetolewa kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kubadilika kwa kufuata Sheria za nchi kwani pasi na hivyo, watafichuliwa kupitia Mfumo wa kisasa wa Kamera za barabarani na mitaani (CCTV) zilizofungwa kwenye maeneo kadhaa ya Jiji la Dodoma wakifanya matendo ya kihalifu na watachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameyasema hayo Septemba 30, 2025 alipokua kwenye ziara ya ukaguzi wa Mradi wa kusimika Kamera za barabarani kwenye maungio ya barabara za kuingia na kutoka Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuimarisha ulinzi ndani ya Jijini hili la Makao Makuu ya nchi.

“Nitoe wito kwa wananchi wa Dodoma wabadilike kwa kufuata sheria na taratibu za nchi kwani wasipofanya hivyo wataonekana kupitia Mfumo wa Kamera za barabarani wakifanya uhalifu na watakapoonekana wakitenda kinyume cha taratibu, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao”.

Aidha, Mhe. Senyamule ameongeza kuwa kupitia Teknolojia hiyo, ufanisi wa kazi kwa Watumishi utaongezeka kwani Kamera hizo zitawekwa kwenye maeneo makubwa na kuleta sifa kwa wageni kuingia na kuwekeza kutokana na uhakika wa usalama hivyo amewaasa wananchi kuilinda miundombinu ya Serikali kwani imewekwa kwa faida yao.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema zoezi hilo lililogharimu kiasi cha shilingi Milioni 473, linaunga mkono juhudi za ujio wa Serikali Mkoa wa Dodoma pamoja na kutimiza ndoto ya Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuifanya Dodoma kuwa sehemu salama kwa uwekezaji na utalii.

Vile vile, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Wislance Smart System Bw. Wisley A. Ussiri ambao wanatekeleza Mradi huo amesema Mradi huo umelenga njia kuu nne za kuingia na kutoka Jiji la Dodoma ambapo utekelezaji wake umefikia 90% na Kamera zilizofungwa ni za kisasa zenye kuleta tija kwani zinaonesha picha zenye ubora wa hali ya juu.

Mradi wa kusimika Kamera za barabarani katika Mkoa wa Dodoma umetumia siku 90 sawa na Miezi mitatu ya utekelezaji ambapo nguzo 50 zilizobeba jumla ya Kamera 106 zenye uwezo wa kutumia teknolojia ya kisasa ya Akili Mnemba zimesimikwa kwenye maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dodoma.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#nimejiandikishanitapigakura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NI SEHEMU NZURI YA UWEKEZAJI

    October 01, 2025
  • CCTV CAMERA KUFICHUA WAVUNJIFU WA SHERIA KATIKA JIJI LA DODOMA

    September 30, 2025
  • DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI KWENYE MICHORO YA MIAMBANI KONDOA

    September 27, 2025
  • JUHUDI KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO ZAPAMBA MOTO

    September 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.