• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JUHUDI KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO ZAPAMBA MOTO

Imetumwa : September 25th, 2025

Na. Sizah Kangalawe

Habari Dodoma Rs

Wadau wa sekta ya Afya wamepongezwa kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kutokomeza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wa umri chini ya Miaka 5.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Septemba 26 Mwaka huu wakati alipotembelea kituo cha afya Ugogoni, Wilayani Kongwa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi Wilayani humo.

"Niwashukuru wadau ambao wameona sababu  ya kushirikiana na Serikali yetu katika kukamilisha eneo hili la kimkakati ambalo linaendana na maono ya Serikali na miongozo yetu. Nchi yetu imekua ikipambana sana kupunguza vifo vya kina mama na watoto.

Hapa naambiwa mama ambaye bahati mbaya mtoto amefariki akiwa tumboni atapata huduma hiyo ambayo isipotolewa kwa umakini inaleta hatari kwa mama, angalau hapa patasaidia kufanya mama huyo apate mazingira rafiki ya kuokoa uhai wake", amepongeza Mhe.  Senyamule

Kituo cha Afya Ugogoni kilipokea fedha kiasi cha Tsh. 23,380,000/= kutoka kwa wadau wa BUFFET FOUNDATION kwaajili ya ujenzi wa jengo maalumu la huduma ya dharura itolewayo kwa ujauzito ulioharibika.

Akizungumza katika eneo la ujenzi wa kituo cha Afya Laikala, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S. Mayeka amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya 6 katika sekta ya Afya.

" Kituo hiki cha afya Laikala kitakuwa ni kituo cha 10 kwenye Wilaya yetu na Katika vituo 10 tulivyonavyo, vituo 6 vimejengwa ndani ya Miaka 4 ya Serikali ya awamu ya sita, kwahiyo unaweza kuona Rais wetu anavyofanya kazi kwa bidii ya kuleta maendeleo", alisema Mhe. Mayeka

Katika ziara hiyo RC Senyamule alitembelea na kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Bweni la Shule ya Sekondari Kimaghai A' na Ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya  Mpwapwa pia ujenzi wa madarasa 2 na matundu ya vyoo  katika  Shule ya msingi Kongwa, ujenzi wa jengo la dharula Kwa wajawazito la kituo cha afya Ugogoni na Ujenzi wa kituo cha afya Laikala.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NI SEHEMU NZURI YA UWEKEZAJI

    October 01, 2025
  • CCTV CAMERA KUFICHUA WAVUNJIFU WA SHERIA KATIKA JIJI LA DODOMA

    September 30, 2025
  • DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI KWENYE MICHORO YA MIAMBANI KONDOA

    September 27, 2025
  • JUHUDI KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO ZAPAMBA MOTO

    September 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.