• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI KWENYE MICHORO YA MIAMBANI KONDOA

Imetumwa : September 27th, 2025

Na; Happiness E. Chindiye

     Habari - Dodoma RS

 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Tanzania Forest Services (TFS) na EPIC Nyama Choma wameadhimisha Siku ya Utalii Duniani Septemba 27, katika eneo la kihistoria la michoro ya miambani ya Kondoa (Kondoa Rock Art).

Katika maadhimisho hayo, washiriki walipata fursa ya kujifunza historia na thamani kubwa ya michoro hiyo ya miambani ambayo imetambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kama urithi wa dunia.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa Bi. Christina Kalezi alitoa salamu na pongezi kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Wadau hao  kwa juhudi zao za kuendeleza na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Dodoma.

“Ninawapongeza kwa kushirikiana kuadhimisha siku hii muhimu katika eneo la kipekee duniani. Michoro ya miambani ya Kondoa ni urithi wa dunia unaotambulisha historia yetu, hivyo ni wajibu wetu sote kuutunza na kuutangaza kwa vizazi vya sasa na vijavyo,” - Amesema  Bi. Christina.

Aidha, amewahimiza washiriki na wadau wa utalii kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa vivutio vya kitalii vilivyopo, hususani Mkoa wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

“Nawasihi kila mmoja awe balozi wa utalii, si kwa wageni wa nje pekee bali hata kwa ndugu na marafiki wa ndani ya Nchi. Utalii wa ndani ukikuzwa vizuri, una nafasi kubwa ya kuchochea uchumi wa jamii na Taifa Letu,” aliongeza.

Hata hivyo ameeleza kuwa  utalii wa kiutamaduni na kihistoria ni nyenzo muhimu ya kukuza uchumi wa jamii na Taifa, hivyo kuna wajibu wa kuvilinda, kuvitunza na kuvitangaza vivutio hivyo.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wadau mbalimbali wa utalii, vijana, pamoja na wanajamii,waliojionea uzuri na upekee wa urithi wa historia ya binadamu uliohifadhiwa katika michoro hiyo ya miambani.


&&&


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#nimejiandikishanitapigakura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NI SEHEMU NZURI YA UWEKEZAJI

    October 01, 2025
  • CCTV CAMERA KUFICHUA WAVUNJIFU WA SHERIA KATIKA JIJI LA DODOMA

    September 30, 2025
  • DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI KWENYE MICHORO YA MIAMBANI KONDOA

    September 27, 2025
  • JUHUDI KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO ZAPAMBA MOTO

    September 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.