• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA NI SEHEMU NZURI YA UWEKEZAJI

Imetumwa : October 1st, 2025

Na Sofia Remmi.

Habari - Dodoma RS

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema kukosekana kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tano kumekuwa kikwazo kwa mikutano mikubwa ya kimataifa kufanyika katika Mkoa huu, licha ya uwepo wa makao makuu ya Serikali.

Mhe. Senyamule amesema hayo tarehe 30/09/2025 alipokuwa akizungumza na wamiliki wa hoteli wa Mkoa wa Dodoma.

Amesema kutokana na hali hiyo sekta binafsi inalo jukumu la kuhakikisha kuwa unafanyika uwekezaji utakaokidhi mahitaji hayo.

"Hivi sasa hatuna hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo zingeweza kutumiwa na wageni wa kimataifa ambao wanakuja Nchini kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Amesema, viwango vya kimataifa vinahitaji uwepo wa hoteli zenye hadhi ya nyota tano zisizopungua tano ndipo kuwa na uwezo wa  kufanyika kwa shughuli hizo katika eneo husika hivyo kutoa wito kwa wawekezaji kutumia fursa hiyo.

"Nitoe wito kwa wawekezaji kuwekeza hoteli zenye hadhi ya nyota tano au mziboreshe zilizopo hivi sasa ili ziweze kufikia hadhi hiyo,  serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana ikiwamo ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato.

"Mikutano mikubwa ya kimataifa huwa inafanyika katika makao makuu ya nchi, lakini hivi sasa hatuwezi kutokana na kukosa hoteli na kumbi kubwa zenye hadhi, hivyo hatuna budi kuwekeza katika sekta hii muhimu, "amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wamiliki wa Hotel Mkoa wa Dodoma Bw.Gabriel Mauna amezipongeza mamlaka za maji na Umeme kwa kufanya maboresho katika sekta zao na kusababisha kurahisishwa kwa huduma hizo muhimu.

“Tunashukuru  Serikali ya Mkoa, kwasababu mara ya mwisho tulipokutana, tulitoa changamoto zetu na mojawapo ilikuwa ni umeme na maji, tunashukuru changamoto hizi zimefanyiwa kazi na katika hili nawapongeza DUWASA na TANESCO kwa kuboresha huduma hizi za muhimu kwetu", amesema Mauna

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NI SEHEMU NZURI YA UWEKEZAJI

    October 01, 2025
  • CCTV CAMERA KUFICHUA WAVUNJIFU WA SHERIA KATIKA JIJI LA DODOMA

    September 30, 2025
  • DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI KWENYE MICHORO YA MIAMBANI KONDOA

    September 27, 2025
  • JUHUDI KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO ZAPAMBA MOTO

    September 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.